Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Neno la wiki-Afueni au Ahueni?

Neno la wiki-Afueni au Ahueni?

Katika neno la wiki tunachambua maneno afueni na ahueni, mchambuzi wetu leo ni, Nuhu Zuberi Bakari ambaye ni Naibu Mwenyekiti wa Maswala ya Mawasiliano kwenye Chama cha  Kiswahili cha Taifa nchini Kenya, CHAKITA. Maneno haya yote yako kwenye kiswahili lakini ni lipi sahihi kutumia?.

Bwana Zuebri anaanza kwa msemo wa kwamba waswahili wanasema afua ni mbili: kufa na kupona kwa maana kwamba neno afua lina maana ya heri ama afadhali. Kwa mfano mtu anaweza kusema kwamba amechoka na kwamba amezingwa na kazi wiki nzima leo ndio amepata afua ama afueni. Nchini Kenya neno linalotumika ni afueni lakini watu walio na mazingira ya pwani kwa mfano: Zanzibar, Mombasa au nchini Tanzania wanatumia neno ahueni, yaani kwamba mtu atasema amepata ahueni.

Zuberi anasema kwamba etimolojia ya neno afueni inatokana na neno afua lakini neno ahua halijui ila yote mawili afueni na ahueni yanatumika kulingana na mazingira.