Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Quartet yazikaribisha Israel na Palestina kurejea tena mezani kwa majadiliano

Quartet yazikaribisha Israel na Palestina kurejea tena mezani kwa majadiliano

[caption id="attachment_288887" align="alignleft" width="430"]barazakuuquartet

Jopo la pande nne kwa ajili ya kusaka amani ya Mashariki ya Kati Quartet limezikaribisha Israel na Palestina kuanza tena majadiliano yenye maana , huku kukiwa na tisho kubwa la amani katika ukanda huo.

Quartet ni mjumuisho wa Umoja wa Mataifa, Marekani, Urusi na Muungano wa Ulaya na ilianzishwa ili kuwa mpatanishi wa mchakato wa amani Mashariki ya Kati. Katika ripoti yake iliyochapishwa Ijumaa imetoa wito kwa pande zote kujihusisha na utekelezaji wa mapendekezo mapya ili kurejesha mchakato wa amani katika njia inayostahili.

Ripoti hiyo inataja mlolongo wa vitisho dhidi ya mchakato wa amani na lengo ya kile ilichokiita suluhu ya mataifa mawili ambapo Israel na Palestina wataishi pamoja. Imetaja pia kuendelea kwa ghasia kupitia ugaidi na uchochezi, kupanuliwa kwa makazi ya walowezi wa Kiyahudi na mamlaka ya Palestina kukosa udhibiti wa Gaza kama ni vikwazo vikubwa.

Quartet imerejea msimamo wake kwamba makazi yoyote ni lazima yakidhi mahitaji ya usalama ya Israel pamoja na kumaliza ukaliaji wa ardhi ya Wapalestina ulioanza mwaka 1967. Unamuzi wowote binafsi wa upande wowote imesema ripoti hautotambuliwa na jumuiya ya Kimataifa.