Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

IOM yatoa ombi kwa ajili ya mgogoro bonde la ziwa Chad na CAR

IOM yatoa ombi kwa ajili ya mgogoro bonde la ziwa Chad na CAR

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, limezindua ombi kwa wahisani ili kushughulikia mgogoro wa kibinadamu kwenye bonde la ziwa Chad uliotawanya watu karibu milioni tatu katika nchi nne na wa Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR uliotawanya watu 400,000. Taarifa kamili na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Machafuko katika bonde la ziwa Chad yalianza 2014, na wanamgambo wa Boko Haram na kusababisha operesheni za kijeshi katika ukanda huo. Maelfu wamepoteza maisha na mamilioni kulazimika kukimbia makwao nchini Nigeria, Niger, Cameroon na Chad.

Mratibu wa misaada ya dharura ameuelezea mgogoro huo kama ni mmoja wa iliyo na ufadhili mdogo kabisa na uliosahaulika kushughulikiwa duniani.