Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zaidi zahitajika kukabili utapiamlo Nigeria

Hatua zaidi zahitajika kukabili utapiamlo Nigeria

Umoja wa Mataifa na wadau wake huko kaskazini-mashariki mwa Nigeria wanahitaji fedha zaidi kuweza kukabili kiwango cha juu cha utapiamlo miongoni mwa watoto walio na umri wa chini ya miaka mitano. Taarifa kamili na Flora Nducha.

(Taarifa ya Flora)

Ofisi ya Umoja wa Mataifa ya usaidizi wa dharura,  OCHA imesema hali inatisha kwani mzozo ulizuia misaada ya kibinadamu kufikia wahitaji, shughuli za uzalishaji zilikoma, masoko yalifungwa na sasa wameweza kufikia wahitaji na kubaini hali ni mbaya hususan jimbo la Borno.

Jens Laerke ni msemaji wa OCHA, Geneva.

(Sauti ya Jens)

“Ombi la fedha Nigeria ili kukabili masuala ya sasa yaliyosababishwa na mashambulizi ya Boko Haram ni  dola Milioni 279 ambapo hadi sasa tumepata asilimia 22 tu. Hata baada ya kupata fedha za CERF bado tunasaka dola Milioni 204 kukidhi  hali ya sasa.”