Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mambukizo ya virusi vya Ukimwi yapungua, Uganda

Mambukizo ya virusi vya Ukimwi yapungua, Uganda

Habari njema kutoka Uganda ni kwamba maambukizi mapya ya virusi vya Ukimwi yamepungua kwa asilimia 88 katika miaka minne iliyopita kutokana na juhudi za kukabiliana na virusi hivyo, amesema Mkurugenzi wa Shiririka la Umoja wa Mataifa linalohusika na  Ukimwi, UNAIDS nchini Uganda , Musa Bungundu kama anavyoarifu John Kibego.

(Taarifa ya Kibego)

Katika mkutano na wanahabariu Jijini Kampala, Bwana Bungundu alisema mambukizo hayo yalipungua kutoka 162,000 katika mwaka 2011 hadi 83,000 ilipofikia Disemba mwaka jana.

Halikadhalika vifo vinavyosababishwa na Ukimwi vilipungua ktuoka 63,000 hadi 28,000.

Bwana Bungundu aliongeza kuwa, idadi ya wanotumia dawa za kupunguza makalai ya virusi vya Ukimwi ilipanda kutoka 329,000 hadi 834,931, huku idadi ya watoto wanaozaliwa na virusi vya ukimiw ikiwa imepungua kutoka 29,000 katika mwaka 2011 hadi 3,200 mwaka jana.