Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Suluhu ya kuwa na mataifa mawili, Israel na Palestina inawezekana

Suluhu ya kuwa na mataifa mawili, Israel na Palestina inawezekana

Amani baina ya watu wa Israel na Palestina inawezekana na kila liwezekanalo lifanywe kuhakikisha hilo, amesema Jumatano Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon.

Ujumbe huo ni kwa ajili ya wote wanaoshiriki mkutano kwenye Umoja wa Mataifa Geneva, ambao unatathimini ni jinsi gani ya kusukuma mbele mchakato wa amani baina ya Israel na Palestina.

Mtazamo wowote wa muafaka wa baadaye ni kuundwa kwa taifa la Palestina kwenye maeneo yanayokaliwa na Israel tangu vita vya Mashariki ya Kati vya mwaka 1976, kwa kile kinachoitwa suluhu ya mataifa mawili.

Muafaka huo unaweza kufikiwa katika mkutano wa kimataifa ambao Israel inaweza kuhudhuria kwa mujibu wa Mohammad Shtayyeh, mshauri wa ngazi ya juu wa Rais wa Palestina Mahmoud Abbas,

(SAUTI YA MOHAMMAD SHTAYYEH)

“Huu ni wakati wa mataifa mawili, na kama sivyo basi Israel itajikuta ni taifa moja lwenye idadi kubwa ya Wapalestina na mwaka 2020 watakuwa asilimi 53 ya watu wote, hivyo Israel itakuwa serikali ya Wayahudi walio wachache, ikiwaongoza Wapalestina walio wengi, Waislam na Wakristo, na hivyo Israel lazima ikabiliane na hali hii halisi, kupoteza demokrasia yake na kuwa taifa la ubaguzi wa rangi”