Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Dunia iitizame tena DRC :Ging

Dunia iitizame tena DRC :Ging

Mratibu wa operesheni za kibinadamu katika Umoja wa Mataifa Joh Ging amesema mgogoro wa jamhuri ya kidemokraSia ya Kongo DRC ni suala linalohitaji kuangaliwa tena na jumuiya ya kimatifa.

Akiongea na waandishi wa habari mjini New York kuhusu ziara yake nchini humo Ging amesema kuna haja ya kuongeza fedha kwa ajili ya kutatua changamoto za kibinadamu zitokanazo na machafuko hayo yanayoathiri mamilioni ya raia.

Kufuatia ziara yake iliyomfikisha Mashariki mwa nchi hiyo kwenye kambi iitwayo Kanabe yenye takribani wakimbizi wa ndani 11,000 wakiwa ni matokeo ya mapigano kati yajeshi la nchi, kikosi cha Umoja wa Mataifa cha kulinda amani MONUSCO na waasi wa FDLR, anaeleza hali ilivyo.

(SAUTI GING)

‘‘Ilikuwa rahisi kushuhudia kwanza namna watu hawa walivyoathirika kwa madhila kimwili na kisaikolojia, mahitaji yao na ukubwa pengo kati ya mahitaji yao na uwezo wa kibinadmau wa kuyashughulikia.’’

Mratibu huyo wa operesheni za kibinadamu katika Umoja wa Mataifa John Ging kadhalika alisafiri hadi Angola kushudia na kutahimini madhara ya El Nino ambapo amesema utapiamlo ni moja ya matokeo ya El Nino