Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajenda mpya ya miji izingatie haki za binadamu kwa kila mtu:UM

Ajenda mpya ya miji izingatie haki za binadamu kwa kila mtu:UM

Kundi la wataalamu 12 wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa, leo wametoa wito wa ajenda mpya ya miji ambayo itatambua ukandamizaji wa haki za binadamu unaosababishwa na ukuaji usio sawia wa kiuchumi mijini na kujitoa kimasomaso kwa kukabiliana na hali ya haki za binadamu, ikiwa ni pamoja udhibiti wa sekta binafsi sambamba na kanuni za haki za binadamu.

Wataalamu hao wanahoji ajenda ya miji ya karne ya 21 ni kwa ajili ya nani? Mbele ya ujumbe wa mataifa mbalimbali waliokutana New York kwa ajili ya kujadili mswada wa ajenda mpya ya miji ambao utapitishwa kwenye mkutano wa Umoja wa Mataifa kuhusu nyumba na maendeleo endelevu, Habitat III, utakaofanyika Oktoba 17 hadi 20 mwaka 2016 jini Quito, Ecuador.

Wanasema endapo haitalenga kuimarisha maisha ya wale wanaoishiki katika umasikini , kwenye hali mbaya katika makazi yasiyo rasmi, endapo haitokuwa kwa ajili ya wale wasio na makazi au kundi ambapo kila mara linakabiliwa na ubaguzi na kutengwa, watu wenye ulemavu, wazee, wanawake, wakimbizi wa ndani, walio wachache, watu wa asili, wahamiaji na wakimbizi, basi ni lazima kujiuliza ajenda hiyo ni kwa ajili ya nani?