Serikali za Afrika zimejizatiti kushughulikia mizozo- AU

29 Juni 2016

Serikali za Afrika zinapaswa kuimairsha ufanisi wao katika kupambana na mizozo ya kibinadamu, wamesema leo wawakilishi wa Afrika waliohudhuria mkutano kuhusu majukumu ya serikali za Afrika katika operesheni za kibinadamu uliofanyika leo mjini New York Marekani. Taarifa zaidi na Assumpta Massoi.

(Taarifa ya Assumpta)

Akihutubia mkutano huo, mtalaam wa masuala ya kibinadamu katika Muungano wa Afrika AU Renny Mike Wafula amesema AU imeshaunda mkakati wa pamoja kwa ajili ya kukabiliana na mizozo ya kibinadamu.

Amesema ili kutimiza dira yake ya maendeleo, bara la Afrika ni lazima lipambane na izizi ya mizozo ya kisiasa, changamoto za kiutawala na madhara ya kibinadamu.

Bwana Wafula amesema katika kipindi cha miaka kumi ijayo Muungano wa Afrika utaanzisha shirika lake la kushughulikia masuala ya kibinadamu.

(Sauti ya Bwana Wafula)

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter