Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Maelfu ya wanawake wajawazito wafurushwa na Boko Haramu Niger

Maelfu ya wanawake wajawazito wafurushwa na Boko Haramu Niger

Maelfu ya wanawake wajawazito wamefurushwa kufuatia mashambulizi ya Boko Haramu . Maelezo zaidi na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Kwa mujibu wa shirika la Umoja wa mataifa la idadi ya watu UNFPA takribani wanawake na wasichana 3000 wajawazito waliotawanywa na mashambulizi hayo wanahitaji msaada wa haraka, wa kliniki, huduma ya kina mama na huduma ya baada ya kujifungua.

Mashambulizi mjini Bosso mapema mwezi huu yamewafungisha virago watu wapatao 75,000, ikiwa ni pamoja na wakazi wote wa Bosso na miji ya jirani ya Toumour and Yebi.

UNFPA inasema wanawake wengi wamelazimika kujifungua porini wakati wakikimbia. Hivi sasa inatoa msaada wa vifaa vya kusaidia kujifungua salama, hali kadhalika vya usafi na vile vya muhimu wakati wa kujifungua.