Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mashirika ya UM yaonya juu ya uhakika wa chakula Sudan Kusini:FAO

Mashirika ya UM yaonya juu ya uhakika wa chakula Sudan Kusini:FAO

Nchini Sudan Kusini watu milioni 4.8 ambao ni theluthi moja ya watu wote wanatarajiwa kuhitaji msaada wa chakula mwezi Julai. Taarifa kamili na Flora Nducha.

(Taarifa ya Flora)

Kukiwa na hatari ya baa la njaa katika baadhi ya sehemu za nchi hiyo , hali inatarajiwa kuwa mbaya zaidi katika miezi ijayo.

Hayo ni kwa mujibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa likiwemo la chakula na kilimo FAO, la mpango wa chakula duniani WFP na la kuhudumia watoto UNICEF.

Erminio Sacco ni mkuu wa ushauri wa kiufundi katika masuala ya uhakika wa chakula FAO aliyeko mjini Juba , anaelezea zaidi kuhusu hali ya sasa nchini humo

(SAUTI YA ERMINIO)

‘Hali hii ni mbaya hakika, tukizingatia historia ya uhakika wa chakula haijawahi kushuhudiwa kabla na inachagizwa na idadi ya watu ambayo inakuwa kwa asilimia tatu kwa mwaka.’’