Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sahel inakabiliwa na umasikini, mabadiliko ya tabia nchi na itikadi kali: UM

Sahel inakabiliwa na umasikini, mabadiliko ya tabia nchi na itikadi kali: UM

Ukanda wa Sahel barani Afrika unakabiliwa na umasikini uliokithiri, unaochangiwa na mabadiliko ya tabia nchi na kuchochewa zaidi na ghasia za itikadi kali.

Haya ni kwa mujibu wa mratibu wa Umoja wa Mataifa wa kikanda kuhusu masuala ya kibinadamu Sahel , ikijumuisha Ziwa Chad na Mali.

Toby Lanzer yuko New York makao makuu ya Umoja wa mataifa kuhudhuria mkutano ulioandaliwa na baraza la kiuchumi na kijamii (ECOSOC) ili kutoa wito wa mshikamano zaidi na ufadhili kuweza kukidhi mahitaji ya kibinadamu yanayoongezeka kila uchao.

Katika ukanda huo wa Sahel watu zaidi ya milioni 23.5 wanakabiliwa na uhakika mdogo wa chakubla , watoto zaidi ya milioni 5.9 wana utapia mlo na watu takribani milioni nne unusu ni wakimbizi wa ndani. Na bwana Lanzer ana ujumbe kwa jumuiya ya kimataifa

(SAUTI YA TOBY LANZER )

"Tunahitaji kuongeza juhudi zaidi, nadhani suala hapa sio tuu kuhusu msaada , ni kuhudu msaada na maendeleo, utetezi , ni jinsi gani sisi hapa kwenye mfumo wa Umoja wa Mataifa, tunaweza kujitahidi kuwahakikishia watu usalama nyumbani wanakotoka ambako wanataka kuwepo."