Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ethiopia sasa mwanachama wa Baraza la Usalama

Ethiopia sasa mwanachama wa Baraza la Usalama

Ethiopia imechaguliwa leo kuwa nchi mwanachama asiye wa kudumu kwenye Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa.

Uchaguzi wa Ethiopia umefanyika leo katika Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, ambapo pia Bolivia, Kazakhstan na Sweden zimechaguliwa kuwa wanachama wasio wa kudumu kwenye Baraza la Usalama, katika kura inayoendelea sasa kumsaka mwanachama wa tano, kati ya Uholanzi na Italia.

Baraza la Usalama lina wanachama 15, ambapo watano – Marekani, Uchina, Uingereza, Ufaransa, na Urusi - ni wa kudumu, wakiwa na uwezo wa kura ya turufu, na kumi wasio wa kudumu, na wasio na uwezo wa kura ya turufu.