Skip to main content

Suluhu ya Kisiasa yahitajika kutanzua zahma ya wakimbizi wa ndani Afrika:Beyani

Suluhu ya Kisiasa yahitajika kutanzua zahma ya wakimbizi wa ndani Afrika:Beyani

Suluhu ya kisiasa yahitajika , ili kutanzua zahma ya wakimbizi wa ndani barani Afrika, kwa mujibu wa mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za binadamu za wakimbizi wa ndani.

Migogoro ya muda mrefu na usalama mdogo vimesababisha mamilioni ya watu kuzikimbia nyumba zao Sudan Kusini, Nigeria, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Jamhuri ya Afrika ya Kati.

Tofauti na wakimbizi, wakimbizi wa ndani wanasalia nchini mwamo. Chaloka Beyani anaeleza ni kwa nini bado kuna wakimbizi wa ndani wengi barani humo.

(SAUTI YA BEYANI)

“Nadhani ni kwa sababu chanzo cha watu kukimbia bado kinaendelea hakijapatiwa ufumbuzi, tunahitaji suluhu ya kisiasa Ili kutanzua hali za kisiasa, na hivyo kuweza kukabiliana na hali ya kibinadamu ya wakimbizi wa ndani”