Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ukosefu wa makazi ni janga la ubinadamu- Mtaalam wa UM

Ukosefu wa makazi ni janga la ubinadamu- Mtaalam wa UM

Mtaalam maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki ya kuwa na makazi, Leilani Farha, amepongeza leo mchakato mkubwa wa wanahabari jijini San Francisco wa kumulika ukosefu wa makazi, ambao umetajwa kuwa janga la ubinadamu.

Mchakato huo unalenga kuibua mijadala kuhusu hali ya watu kutokuwa na makazi na kuhamasisha umma, pamoja na kuonyesha jinsi serikali zinavyoshindwa kutekeleza wajibu wao, na hivyo kuwaondolea lawama watu binafsi wanaokosa makazi.

Katika mchakato huo wa siku tano, vyombo 70 vya habari mashinani na kwenye ngazi za kitaifa na kimataifa, vitachapisha hadithi za watu wasio na makazi na kinachosababisha hali hiyo.

Bi Farha amesema kuonyesha watu wasio na makazi katika vyombo vya habari kunaweza kubadili mtazamo wa umma kuhusu hali hiyo na kuibua moyo wa huruma.