Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Athari za El Niño Afrika ni kubwa:OCHA

Athari za El Niño Afrika ni kubwa:OCHA

Mashariki na kusini mwa Afrika watu takribani milioni 50 wana matatizo ya uhakika wa chakula , wengi wao ikiwa ni kutokana na ukame wa muda mrefu uliochangiwa na El Niño au mchanganyiko wa vita na ukame.

Hayo ni kwa mujibu wa ripoti ya tathimini ya athari za El Niño kwa Afrika iliyofanya na shirika la Umoja wa mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura OCHA.

Shirika hilo linasema Kusini mwa Afrika inakadiriwa kwamba watu milioni 21.7 watahitaji msaada wa chakula , na wadau wa misaada wanapanga kuwasaidia watu milioni 12.8 katika mataifa yaliyoathirika zaidi ya Angola, Lesotho, Madagascar, Malawi, Msumbiji, Swaziland na Zimbabwe. Mataifa mengine yanayohitaji msaada ni Ethiopia, Sudan na Somalia.