Skip to main content

IOM yatoa mafunzo kwa maafisa wa afya mipakani kukabili homa ya manjano DRC

IOM yatoa mafunzo kwa maafisa wa afya mipakani kukabili homa ya manjano DRC

Kwa ombi maalumu kutoka mpango wa kitaifa wa usafi mipakani nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, shirika la kimataifa la uhamiaji IOM linatoa mafunzo kwa kundi la kwanza la maafisa wa afya mipakani, kama sehemu ya mkakati wa kitaifa kukabiliana na mlipuko wa homa ya manjano nchini humo.

Mafunzo hayoa yameendeshwa mjini Matadi kwenye mpaka na Angola na kuhudhuriwa na maafisa wa afya 25 kutoka uwanja wa ndege wa Kinshasa, kutoka Ngobila kwenye mto Congo ma vituo vingine vikubwa vya mpakani vya Mbanza Ngungu, Kimpese Lufu, Ango-Ango (Matadi), Boma, Lindu, Yema, Yatch na Moanda.