Zeid alaani chuki dhidi ya wageni Uingereza

28 Juni 2016

Kamishna Mkuu wa haki za binadamu katika Umoja wa Mataifa Zeid Ra’ad Al Hussein amelaani vikali taarifa ya za mashmbulizi yanayotokana na chuki dhidi ya wageni nchini Uingereza.

Akiongea mjini Genenva Uswisi, Kamishna Zeid amesema vitendo hivyo vya mashambulizi ya hivi karibuni ambapo walengwa wamekuwa ni jamii ndogo na raia wa kigeni hayakubaliki kwani ni ubaguzi na chuki dhidi ya wahamiaji  na kuzitaka mamlaka za Uingerrza kuchukua hatua stahiki.

Wakati huo huo mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu aina mbalimbali za ubauguzi, na chuki dhidi ya wageni Mutuma Ruteere amezungumza hii leo mjini Geneva Uswisi akikemea vitendo hivyo vinavyodhalilisha utu wa binadamu.

(SAUTI RUTEERE)

‘‘Imebainika kwamba wahamiaji ni wahanga wa ubaguzi kwa sababu kabila au dini zao mara nyingi hutofautiana na wenyeji. Wanawake wahamiaji mara nyingi hukumbana na unyanyasaji katika maeneo ya kingono, kikabila  na hadhi za uhamiaji

 

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter