Wakimbizi wanapatiwa taarifa kuhusu hali ilivyo Somalia kabla ya kufanya maamuzi
Nchini Kenya harakati zinaendelea kuwawezesha wakimbizi 320,000 kutoka Somalia walioko kambi ya Dadaab kurejea nyumbani. Hiyo ni kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi duniani, UNHCR ambalo ni moja wa pande tatu za kamisheni ya kuwarejesha kwa hiari wakimbizi waSomali kutoka Kenya.
Pande tatu hizo ikiwemo serikali ya Kenya, ile ya Somalia na UNHCR, wamefanya mazungumzo kwa lengo la kuona kwamba wakimbizi 150,000 wanarejea Somalia kwa hiari na kwa njia yenye hadhi na katika mazingira salama mwaka huu wa 2016.
Je hatua zimefika wapi? Basi ungana na Grace Kaneiya wa Idhaa hii katika mahojiano na Duke Mwancha, Kaimu Msemaji wa UNHCR nchini Kenya.