Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuna matarajio ya kuongeza kasi ya usaidizi wa kibinadamu: O'Brien

Tuna matarajio ya kuongeza kasi ya usaidizi wa kibinadamu: O'Brien

Mjadala wa masuala ya kibinadamu umefunguliwa leo mjini New York ambapo wadau wa maendeleo wataangazia pamoja na mambo mengine mahitaji ya usaidizi wa kibinadamu.

Mjadala huo wa juma moja uko chini ya uenyeji wa baraza la uchumi na masuala ya kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC ambapo zaidi wawakilishi kutoka takribaji nchi 180 wanashiriki.

Akiongea wakati wa mahojiano na redio ya Umoja wa Mataifa muda mfupi kabla ya uzinduzi , Mkuu wa Ofisi ya kuratibu masuala ya kibinadamu na misaada ya dharura katika Umoja wa Mataifa (OCHA), Stephen O'Brien amesema mkutano huo ni muhimu kwani katika dunia ya leo kila mtu ana mahitaji ya kibinadamu wakati wa dharura.

Amesema umuhimu wa mkutano huu ni.

( SAUTI O’BRIEN)

‘Tuna matamko ya ajabu kuhusu matarajio pamoja na wale wanaotoa misaada ya kibinadamu duniani. Zaidi ya yote kuongeza kasi ya utekelezaji wa ahadi ya kutoa misaada ya kibinadamu kwa wahitaji.’’