Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Changamoto zinazowakabili wajane na juhudi za usaidizi Tanzania

Changamoto zinazowakabili wajane na juhudi za usaidizi Tanzania

Siku ya kimataifa ya wajane ambayo huadhimishiwa kila Juni 23, mwaka huu imejikita katika kuhakikisha ustawi wa kundi hilo ambalo mara kadhaa hukumbana na mateso katika jamii.

Takwimu zinaonyesha kuwa kuna takribani wajane milioni 259 duniani kote na karibu nusu wanaishi katika hali ya umasikini. Umoja wa Mataifa unatetea haki za kundi hilo linalonyanyapaliwa na familia zao na jamii huku wengine wakikumbwa na ubaguzi sababu ya umri na jinsia.

Kufahamu hali ilivyo Tanzania ungana na Nicholas Ngaiza wa redio washirika Kasibante Fm ya Kagera Tanzania anayemulika madhila na usaidizi kwa wajane.