Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ECOSOC yajadili chagamoto za usaidizi wa kibinadamu

ECOSOC yajadili chagamoto za usaidizi wa kibinadamu

Baraza la kiuchumi na kijamii la Umoja wa Mataifa ECOSOC leo limekuwa na mkutano wa kujadili masuala ya usaidizi wa kibinadamu likizingatia ajenda 2030 ya maendeleo endelevu SDGs yenye shabaha ya kuwajumuisha watu wote.

Akiongea katika mkutano huo kwa njia ya video kutoka Lebanon kuhusu changamoto za kibinadmau zinazoiukumba nchi hiyo ambayo ni moja ya nchi zinazobeba mzigo mkubwa kwa kuhifahdi wakimbizi wa Syria Dk Kalil Gebara ambaye ni mshauri wa waziri wa mambo ya ndani wa Lebanon anasema.

(SAUTI DK GEBARA)

''Leo Lebanon inakabiliwa na changamoto nyingi zilizo juu ya uwezo wa nchi kiuchumi, kijamii na hata idadi ya watu katika kupata upenyo wa janga hili.''

Awali washiriki wa mkutano huo walitizama video kuhusu changamoto za kibinadamu nchini Lebanon nchi inayohifadhi wakimbizi wa Syria na juhudi za usaidizi