Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UM Tanzania wazindua mpango wa maendeleo.

UM Tanzania wazindua mpango wa maendeleo.

Ofisi ya Umoja wa Mataifa nchini Tanzania, imezindua awamu ya pili ya mpango wa usaidizi maendeleo UNDAF uanolenga kusaidia kusukuma mbele juhudi za maendeleo katika sekta tofauti nchini humo.

UNDAF awamu ya pili inaanzia mwaka 2016 hadi 2021.

Wakiongea baada ya uzinduzi huo mjini Dar es salaam Katibu Mkuu wa wizara ya elimu na mafunzo ya ufundi Profesa Sifuni Mchome ameelezea namna taifa litakavyonufaika na mpango huo.

(SAUTI MCHOME)

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa wizara ya fedha na mipango wa Zanzibar Khamis Musa anazungumzia namna mpango wa awali ulivyofanikiwa.

( SAUTI KHAMIS)

Zaidi ya dola bilioni moja za Kimarekani zimetengwa kwa ajili ya mpango huo wa maendeleo wa Umoja wa Mataifa wa awamu ya pili UNDAF.