Umuhimu wa mabaharia utambuliwe : IOM

25 Juni 2016

Baharini kwa wote ni kauli mbiu inayotumika kwa ajili ya kuadhimisha siku ya kimataifa ya mabaharia leo Juni 25, 2016.

Shirika la kimataifa la uhamiaji IOM, linaadhimisha siku hii kwa mara ya sita kwa kuangazia umuhimu wa mabaharia katika bahari duniani ambapo Katibu Mkuu wa IOM Kitack Lim amekaririwa akisema mabaharia hawatambuliwi huku wakitimiza jukumu muhimu la kuisongesha dunia.

Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon katika ujumbe wa kuadhimisha siku hii amesema mabaharia wanalisha dunia, huvalisha na kuihifadhi.

Ban amesema wana umuhimu katika kukuza uchumi jumuishi na aunaojali mazingira.

Sherehe za siku ya mabaharia zitafanyika rasmi Septemba 29 ambayo ni siku ya kimataifa ya masuala ya bahari,ambapo umuhimu wa dhana hiyo utamulikwa.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter