Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Libya: UM walaani mashambulizi ya karibuni kwenye kituo cha afya Benghazi

Libya: UM walaani mashambulizi ya karibuni kwenye kituo cha afya Benghazi

Kufuatia matukio matatu katika siku chache zilizopita ambayo yamefanya fursa za huduma ya afya Benghazi kushambuliwa, naibu mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu na mwakilishi wa shirika la afya duniani WHO, Dr. Syed Jaffar Hussain, wameelezea hofu yao na kuzitaka pande zote kujizuia kulenga vituo vya afya na kuchukua tahadhari zote kuzuia vifo miongoni mwa wagonjwa na wauguzi wa afya.

Akirejerea wajibu wa kwanza wa kuhakikisha wanaheshimu misingi na sheria za kimataifa za masuala ya kibinadamu kwa kuzingatia azimio la baraza la usalama namba 2286, naibu mratibu huyo amelaani vikali vitendo hivyo vya ghasia, mashambulizi na vitisho dhidi ya wahudumu wa afya na watoa misaada ya kibinadamu , wanaojihusisha na huduma za afya, usafiri wao, vifaa vyao pamoja na majengo mengine ya afya.

Amesema mashambulio hayo yanahatarisha zaidi maisha ya wagonjwa na wahudumu ambao tayari wako hatarini na kazi wanaoyoifanya ni muhimu sana katika kuokoa maisha ya wengine.