Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama lakaribisha makubaliano ya amani Colombia

Baraza la usalama lakaribisha makubaliano ya amani Colombia

Wajumbe wa baraza la usalama la Umoja wa Mataifa,  wamekaribisha makubaliano ya kihistoria yaliyofikiwa leo mjini Havana nchini Cuba kati ya serikali ya Colombia na kikundi cha FARC-EP.

Wajumbe hao katika taarifa yao wamepongeza adhma ya pande hizo kinzani katika kufikia makubaliano hayo na kutambua kuwa wanawasilisha hatua muhimu katika kufikia makubaliano ya mwisho ya amani ya kukomesha machafuko nchini Colombia yaliyodumu kwa zaidi ya miaka50.

Wajumbe kadhalika wametambua wajibu muhimu uliochukuliwa na Cuba na Norway kama wadhamini pamoja na Chile na Bolivia katika kufanikisha makubaliano hayo ya amani.

Wamekariri wajibu wao katika mchakato wa amani Colombia na kusisitiza usaidizi katika utekelezwaji wa makubaliano ya amani nchini Colombia kwa mujibu wa azimio namba 2261 la mwaka 2016.