Waethiopia 19 wapoteza maisha ndani ya lori la wasafirishaji haramu wa watu:IOM

24 Juni 2016

Takribani Waethiopia 19 wamekutwa wamekufa ndani ya lori nchini Zambia baada ya kukosa hewa . Lori hilo linasadikiwa kuwa ni la mtandao wa usafirishaji haramu wa binadamu na lilikuwa likielekea Afrika ya Kusini.

Kwa mujibu wa shirika la kimataifa la uhamiaji IOM , wahanga hao walikutwa baada ya manusura kugongagonga kontena walimokuwa wakihitaji msaada. Msemaji wa IOM Joel Millman amesema tukio hilo ni baya sana kulishuhudia.

(SAUTI YA JOEL MILLMAN)

Hili ni kubwakabisa tunalolifahamu, lakini kumekuwa na visa vingine vya kutisha kwatika safari hizo siku za nyuma.Nadhani ilikuwa mwaka jana au miwili iliyopita kulikuwa na tukio la wahamiaji kuzama, ambao walishuhudiwa wakiliwa na mamba, lakini hatujawahi kuona vifo vya kukosa hewa kwenye kontena kama hivi”

Kwa mujibu wa IOM manusura 76 waliojumuisha watoto, wamepelekwa kwenye makazi ya dharura.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter