Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban amteua Ivan Šimonoviæ kuwa mshauri wake maalum kuhusu jukumu la ulinzi

Ban amteua Ivan Šimonoviæ kuwa mshauri wake maalum kuhusu jukumu la ulinzi

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo ametangaza uteuzi wa Ivan Šimonoviæ wa Croatia kuwa mshauri wake maalum kuhusu jukumu la ulinzi.

Taarifa ya msemaji wa Katibu Mkuu imesema Bwana Šimonoviæ amechukua nafasi ya Jennifer Welsh wa Canada ambapo Katibu Mkuu amemshukuru kwa uongozi wake wa kipekee na ushauri kuhusu maendeleo na utekelezaji wa jukumu la ulinzi.

Mteule huyo mpya kwa sasa ni msaidizi wa Katibu Mkuu kuhusu masuala ya haki za binadamu na mkuu wa ofisi ya kamishna wa haki za binadamu mjini New York. Anatarajiwa kuanza rasmi jukumu hilo mnamo Oktoba mosi mwaka huu.

Taarifa hiyo imesema Bwana Šimonoviæ atafanya kazi chini ya muongozo wa mshauri maalum wa Katibu Mkuu kuhusu kuzuia mauaji ya kimbari.