Nchi zinazobeba wakimbizi zinahitaji kusaidiwa:Rodriguez

Nchi zinazobeba wakimbizi zinahitaji kusaidiwa:Rodriguez

Nchi zinazopokea na kuhifadhi wakimbizi zinahitaji kusaidiwa kimataifa kwa manufaa ya wakimbizi lakini pia wenyeji wanaowapokea. Hayo yamesemwa na mratibu mkazi wa Umoja wa Mataifa mjini Dar es salaam nchini Tanzania Alvaro Rodriguez.

(SAUTI RODRIGUEZ)

Kwa upande wa Tanzania imepokea zaidi ya wakimbizi 140,000 wa Burundi kwa kipinzi cha zaidi ya mwaka mmoja tu kutokana na mtafaruku wa kisiasa nchini humo. Hili lina gharama kubwa kwa usalama wa watu na masiha yao, na pia lina gharama kubwa za kiuchumi katika nchu husika kupokea wakimbizi, na linahitaji rasilimali za kutosha ili kuhakikisha watu hawa wanaendelea kuishi maisha yao ya kiutu na ni vigumu sana ukiwa mkimbizi.

Ili kuhahikisha hakuna anayesalia nyuma katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu wakiwemo wakimbizi ametoa wito

(SAUTI RODRIGUEZ)

Ni wito kwa serikali kushughulikia changamotowalizonazo zamsukosuko wa kisiasa , wito wa kuchagiza amani kwa jumuiya ya kimataifa, lakini pia ni wito kwa raia wote wa dunia kuelewa kwamba tunapoingia utekelezaji wa maelengo ya maendeleo endelevu , tunahitaji kuhakikisha hakuna anayeachwa nyuma. Na wakimbizi kuliko mtu mwingine yeyote wanakuna na madhila wanapokimbia nchi zao na wanahitaji msaada wetu.