Baraza la usalama laongeza muda wa vikwazo vya kusafirisha silaha DRC

23 Juni 2016

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limepitisha azimio la kuongeza muda wa vikwazo vya usafirishaji wa silaha nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo, DRC.

Muda umeongezwa hadi tarehe Mosi Julai mwaka 2017 ambapo azimio hilo limeweka bayana kuwa vikwazo havihusishi silaha au vifaa vinavyohusiana na mafunzo au usaidizi kutoka ujumbe wa Umoja wa Mataifa nchini humo, MONUSCO au kikosi cha pamoja cha Afrika.

Halikadhaliki havigusi vifaa vya kujilinda ambavyo vinapelekwa nchini humo na Umoja Mataifa kwa ajili ya kufanikisha kazi zake.

Kuongeza muda kumezingatia kuendelea kuzorota kwa usalama hususan mashariki mwa DRC, ambapo mwakilishi wa kudumu wa DRC kwenye Umoja wa Mataifa, Ignace Gata Mavita amesema..

(sauti ya Mavita)

“Ujumbe wangu unatambua azimio hili lililopitishwa na Baraza la Usalama. Tunashukuru kwa hatua hi ambayo kwa mara nyingine tena inadhihirisha azma yake ya kuimarisha amani kwenye nchi yangu.”

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter