Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkimbizi mwenye ulemavu ahaha kutwa kucha kusaka riziki kutunza familia

Mkimbizi mwenye ulemavu ahaha kutwa kucha kusaka riziki kutunza familia

Ghasia zinazoendelea nchini Syria zinaendelea kuvurumisha wananchi kusaka hifadhi nchi jirani na hata mabara mengineyo ikiwemo Ulaya. Miongoni mwao ni Firaz ambaye yeye na familia yake ya mke na watoto Sita wamepata hifadhi nchini Uturuki.

Maisha ya ugenini ni magumu, na hali inakuwa mbaya zaidi kwa kuwa yeye ana ulemavu. Lakini hiyo haimzuii kusaka riziki kila uchao. Je anafanya nini? Assumpta Massoi amekuandalia makala hii iliyowezeshwa kutokana na usaidizi wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR.