Mtaalamu aonya mauaji ya watu wa asili Brazil

Mtaalamu aonya mauaji ya watu wa asili Brazil

Mtaalamu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu haki za watu wa asili Victoria Tauli-Corpuz, amelaani vikali mauaji ya hivi karibuni ya jamii ya watu wa asili nchini Brazil.

Katika taarifa yake kuhusu mauaji hayo yaliyolenga jamii ifahamikayo kwa jina la Guarani Kaiowá, mtaalmu huyo maalum ametaka mamlaka za kitaifa nchini humo kuchukua hatua za dharura kuzuia mauaji zaidi.

Pia ametaka mamlaka hiyo kufanya uchunguzi dhidi ya mauaji ya watu wa asili Brazil, na kuwawajibisha watekelezaji.

Mnamo Juni 14 mwaka huu, wafanyakazi wawili wa sekta ya afya walipigwa risasi na kufariki dunia, huku watu wengine sita wa jamii asilia wakijeruhiwa kwa risasi akiwamo mtoto wa miaka 12.