Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP imezindua operesheni ya dharura kwa Wamisri wanaorejea toka Libya

WFP imezindua operesheni ya dharura kwa Wamisri wanaorejea toka Libya

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP leo limetia saini waraka wa makubaliano na wizara ya mambo ya nje kwa ajili ya operesheni za dharura za miezi mitatu kuwasaidia Wamisri wanaorejea nyumbani kutoka Libya kwa msaada wa chakula wanaouhitaji.

Operesheni hiyo ya dharura imezinduliwa kwa ombi maalumu la serikali ya Misri , ili kutoa msaada kwa watu 60,000 wanaorejea kutoka Libya katika majimbo matano ya Sohag, Menia, Assuit, Qena na Kafr El Sheikh, ambako idadi ya wanorejea ni kubwa sana.

Vocha ya chakula ya dola 13 kwa mwezi inazipa familia orodha ya bidhaa muhimu za chakula kama nafaka, mafuta na kunde ambavyo wana uhuru wa kuchagua na kwa kiasi chochote wanachotaka kwa jumlya ya vocha walizonazo.

Kwa mujibu wa wizara ya mambo ya nje ya Misri , Libya inahifadhi takribani Wamisri milioni 1.6, wengi wakiwa wafanyakazi wahamiaji.