Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Siasa ndiyo njia ya kutafuta amani, siyo vita- Balozi Kamau

Siasa ndiyo njia ya kutafuta amani, siyo vita- Balozi Kamau

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, leo limefanya kikao kuhusu ujenzi wa amani na uendelezaji wa amani. Taarifa kamili na Joshua Mmali

(TAARIFA YA JOSHUA)

Kwenye kikao cha leo, Baraza la Usalama limehutubiwa na mwenyekiti wa zamani wa Kamisheni ya Ujenzi wa Amani, Balozo Olof Skoog, na mwenyekiti wa sasa, Balozi Macharia Kamau wa Kenya, ambaye amewasilisha ripoti ya kila mwaka ya Kamisheni hiyo.

Akirejelea maazimio ya Baraza la Usalama miezi miwili iliyopita, Balozi Kamau amesema kuendeleza amani ni jukumu la pamoja linaloshirikisha serikali na wadau wa kitaifa, lakini pia linalohitaji uungwaji mkono kwa ngazi ya kimataifa, kwa nchi zilizoko kwenye mizozo au zinazokabiliwa na hatari ya mizozo.

Awali, akihojiwa na idhaa hii kabla ya mkutano wa leo, Balozi Kamau amesema..

(Sauti ya Balozi Kamau)