Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kaag ashuhudia madhila ya wakimbizi wa kipalestina, Lebanon

Kaag ashuhudia madhila ya wakimbizi wa kipalestina, Lebanon

Mratibu maalum wa Umoja wa Mataifa kuhusu Lebanon, Sigrid Kaag ameelezea wasiwasi wake kuhusu mazingira duni ya wakimbizi wa kipalestina walioko kwenye kambi ya Rashidieh, kusini mwa nchi hiyo.

Amesema hayo baada ya kutembelea kambi hiyo na kupata fursa ya kuzungumza na wawakilishi ambao walimweleza masahibu yao ikiwemo hali ngumu ya kiuchumi na kijamii.

Kutokana na hali hiyo Bi. Kaag amesema Umoja wa Mataifa kupitia shirika lake la kusaidia wakimbizi wa kipalestina, UNRWA, utaendelea kusaidia wakimbizi hao waliopatiwa hifadhi Lebanon.

Akiwa kambini hapo, mratibu huyo wa Umoja wa Mataifa alitembelea pia kituo cha afya, kituo cha wanawake pamoja na shule.