Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha juhudi za amani za serikali ya Mali

Ban akaribisha juhudi za amani za serikali ya Mali

Katika maadhimisho ya mwaka wa kwanza wa mkataba wa amani na maridhiano nchini Mali, Katibu Mkuu wa Umoja wa mataifa Ban Ki-moon amekaribisha hatua na jitihada za Rais wa Mali Ibrahim Boubakar Keïta, na serikali yake.

Amesema anatambua na kuridhika na uamuzi wa Rais wa kumteua bwana Mahamadou Diagouraga kama mwakilishi wa kufuatilia mkataba , lakini vile vile utiaji saini wa serikali na makundi yenye silaka mchakato wa makubaliano kuhusu serikali ya mpito na mipango mingine.

Ban amesema haya ni ya muhimu katika kusonga mbele kwenye taifa hilo. Amesema anaamini pande zilizotia saini zitahakikisha utekelezaji wa mkataba huo bila mushikeli wowote , kwa kuzingatia changamoto zilizo mbele yao.

Ban amepongeza wapatanishi katika mchakato huo hususani mwenyekiti Algeria kwa kuunga mkono juhudi hizo za amani.