Tahadhari dhidi ya Zika kwa waendao Brazil- WHO

Tahadhari dhidi ya Zika kwa waendao Brazil- WHO

Shirika la Afya Duniani(WHO) limetoa tahadhari ya afya kwa wote wanaokwenda kwenye mashindano ya Olimpiki nchini Brazili kufuatia mlipuko wa homa ya Zika. Amina Hassan na taarifa kamili..

(TAARIFA YA AMINA)

WHO imesema wasafiri wote pamoja na wachezaji wa mashindano ya olimpiki na Olimpiki ya walemavu lazima wafahamishwe kuhusu hatari za kiafya kwenye maeneo watakayozuru nchini Brazili, lakini pia njia za kujikinga ili kupunguza hatari ya kupata virusi hivyo.

Limeongeza kuwa kila nchi sasa ina ushauri wa kitaifa kuhusu mlipuko wa Zika na wasafiri ni muhimu kupata ushauri kwa mlaka za afya za nchi zao, lakini pia limesema miongoni mwa mambo ya kuzingatia ni watu kujizuia kushika ujauzito kwa kipindi chote watakachokuwa Brazili.

Na kwa upande wa mwenyeji wa mashindano Brazil wizara yake ya afya imejiandaa na inatoa ushauri kwa wageni wote wanaowasili nchini humo ikiwa ni pamoja na kuanzisha tovuti maalumu inayoelezea athari za Zika na jinsi ya kujikinga. Michuano ya Olimpiki inaanza Agosti 5 hadi 21 mwaka huu.