Nchi za Afrika ya Kati zaimarisha mkakati wa kupunguza hatari ya majanga

21 Juni 2016

Wabunge kutoka mataifa ya Afrika ya Kati wanaongeza juhudi za kikanda kukabili athari za majanga ya asili na yale yanayosababishwa na binadamu, kwa kutekeleza mkataba wa Sendai wa upunguzaji hatari ya majanga.

Mtandao wa wabunge kwa ajili ya kudhibiti majanga Afrika ya Kati (REPARC) ulianzishwa mwezi Ocktoba mwaka jana kushughulikia upunguzaji wa hatari ya majanga na mabadiliko ya tabianchi katika mataifa 11 ya jumuiya ya Kiuchumi ya Afrika ya Kati (ECCAS).

Mataifa hayo ni pamoja na Burundi, Cameroon, Jamhuri ya Afrika ya Kati , Chad, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo DRC, Congo Brazzaville, Equatorial Guinea, Gabon na São Tomé and Príncipe.

Kwa majanga makubwa mawili yamekuwa yakiripotiwa kila wiki Afrika Kusini mwa jangwa la Sahara, tangu mwaka 2000 na kuaathiri takribani watu milioni 12.5 kila mwaka. Majanga hayo ni pamoja na mafuriko, vimbunga,na moto wa msituni.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter