Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kubinafsisha usalama kusishushe viwango vya ulinzi na uwajibikaji

Kubinafsisha usalama kusishushe viwango vya ulinzi na uwajibikaji

Mwakilishi maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu, ukiuwaji wa sheria unyongaji au mauaji ya kiholela, Christof HEYNS, leo ametoa wito wa kuchunguza zaidi na uwajibikaji wa matumizi ya nguvu na watoa usalama binafsi katika shughuli za utekelezaji wa sheria.

Katika ripoti yake ya ya hitimisho kwa baraza la haki za binadamu, Bwana Heyns ameonya kwamba kutofuatiliwa au matumizi mabaya ya nguvu kwa makampuni binafsi ya ulinzi na usalama yanaweza kuhatarisha ulinzi wa haki ya kuishi.

Ameyataka mataifa yote kuhakikisha kwamba sheria zao zinazosimamia usalama binafsi ndani na nje zinakwenda shanjari na viwango vya kimataifa vya haki za binadamu na utendaji bora kuhusu matumizi ya nguvu, na lazima kuhakikisha kwamba watoa ulinzi hao wako chini ya uangalizi na uwajibikaji.

Mtaalamu huyo amesema anatambua kwamba makampuni binafsi ya ulinzi yana faida , lakini aksisitiza kwamba waklati huohuo sekta hiyo binafsi ina changamoto kubwa, hasa ukizingatia kwamba nchi zina wajibu wa kutekeleza haki za binadamu , na hivyo kuhishsa zaidi makampuni binafsi ya ulinzi kunazusha maswali hasa katika jukumu, wajibu na uwajibukaji kuhusiana na ukiukwaji wa haki za binadamu na ukatili.