Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kampeni #SharetheMeal yapata mafanikio mengi wakati wa Ramadhan

Kampeni #SharetheMeal yapata mafanikio mengi wakati wa Ramadhan

Kampeni ya #sharetheMeal ya Shirika la Umoja wa Mataifa la Mpango wa Chakula WFP inayowezesha mtu kuwalipia watu chakula imetimiza malengo yake kwa kipindi cha wiki saba tu.

WFP imesema hayo leo ikieleza kwamba tayari imeweza kuhakikisha chakula cha mwaka mzima kwa watoto wakimbizi wa Syria 1,400 waliopo nchini Lebanon. WFP imeeleza kwamba mafanikio hayo yamesababishwa na michango ya watu 20,000 wakati wa mwanzo wa mwezi wa Ramadhan kupitia tafsiri yake ya kiarabu.

Tayari WFP imeweka malengo mapya, ikilenga kusaidia watoto wengine wa Syria 1,500 waliopo nchini Lebanon kwenye kambi za wakimbizi.

Apu ya Share The Meal imezinduliwa Novemba mwaka 2015 na tayari watu 550,000 wamechagia milo zaidi ya milioni 6 duniani kote, kampuni ya Google ikitambua apu hiyo kama moja ya apu bora za mwaka 2015.