Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Msafara wa madaktari wasio na miaka washambuliwa CAR, mratibu alaani

Msafara wa madaktari wasio na miaka washambuliwa CAR, mratibu alaani

Mratibu wa masuala ya kibinadamu wa Umoja wa mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR amelaani vikali mashambulizi dhidi ya msafara wa madaktari wasio na mipaka, MSF nchuni humo, Dr. Michel Yao.  Shambulio la kwanza limefanyika Juni 17 kati ya eneo la Sibut na Grimari mjini Kemo na kukatili maisha ya mkuu wa msafara, na wafanyakazi wengine wakafanikiwa kukimbilia msituni. Waliotekeleza shambulio hilo ni watu wenye silaha wasiojulikana.

Msafara huo ulikuwa unasafirisha dawa na mafuta kutoka mji mkuu Bangui kuelekea Bangassou.

Dr. Yao amesema shambulio linguine limetokea karibu na Bossangoa Juni 18 na kukatili maisha ya dereva wa MSF.

Ameongeza kuwa mashambulio haya ya kikatili yanadhihirisha hali halisi ya kutokuwepo kwa usalama barabarani jambo ambalo linafanya kuwa ngumu sana kazi ya watoa misaada ya kibinadamu kwa maelfu ya watu wanaohitaji msaada huo.