Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WHO yatoa kibali cha awali kwa teknolojia mbili za kubaini VVU kwa watoto wachanga

WHO yatoa kibali cha awali kwa teknolojia mbili za kubaini VVU kwa watoto wachanga

Shirika la afya ulimwenguni, WHO limetoa kibali cha awali kwa teknolojia mbili za aina yake zinazoweza kubaini Virusi Vya Ukimwi, VVU kwa watoto wachanga ndani ya muda mfupi.Taarifa kamili na Grace Kaneiya.

(Taarifa ya Grace)

Mbinu hizo moja iitwayo Alere™ q HIV-1/2 Detect iliyobuniwa na kampuni ya Alere na ile ya HIV-1 Qual Assay kutoka Cepheid AB zinaweza kubaini VVU kwa mtoto hata chini ya saa moja badala ya kusubiri sampuli kupelekwa maabara ambako yaweza kuchukua wiki au hata mwezi kupata majibu.

Mike Ward kutoka kitengo cha kanuni cha WHO kuhusu dawa muhimu amesema hatua hii ni ya muhimu sana katika harakati za kudhibiti Ukimwi miongoni mwa watoto.

Amesema mbinu hizo ni rahisi, haraka na hazihitaji miundombinu ya hali ya juu kama mbinu zilizopo na zinaweza kutumiwa katika eneo lolote la huduma ya afya.

Kupitishwa kwa mbinu hizo kunafuatia majaribio ya mwaka mmoja na nusu kwa ushirikiano baina ya WHO, Afrika Kusini na Marekani.