Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ajenda ya 2030 haitofikiwa makundi ya wachache kama Albino yakibaki nyuma:Mahiga

Ajenda ya 2030 haitofikiwa makundi ya wachache kama Albino yakibaki nyuma:Mahiga

Kongamano la siku tatu la kimataifa kwa ajili ya kutafuta mbinua za kukabiloiana na unyanyapaa, ukatili na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi au Albino limemalizika leo mjini Dar Es salaam Tanzania.

Kongamano hilo la kwanza la aina yake limewaleta pamoja wawakilishi wa serikali , asasi za kiraia, makundi ya watu wenye ulemavu wa ngozi, Umoja wa Mataifa na waandishi wa habari.

Akizungumza kwa niaba ya serikali ya Tanzania wakati wa kufunga kongamano hilo , waziri wa mambo ya nje wa taifa hilo Balozi Augustine Mahiga amesema anatumai limefungua njia ya kuhakikisha hakuna atakayeachwa nyuma katika kufikia malengo ya maendeleo endelevu hususani watu wenye ulemavu wa ngozi na walio wachache.

(SAUTI YA MAHIGA)

"Tunaamini kwamba kuna faida kubwa kwa kuunda ushirika na jamii, viongozi wa kidini na asasi za kiraia. Na ni matumaini yangu kwamba kutokana na kongamano hili tumeweza kufungua njia ya kuimaimarisha ushirikiano wetu wa kikanda katika kushughulikia masual ya watu wenye ulemavu ngozi Afrika, sambamba na utekelezaji wa ajenda ya 2030 ya maendeleo endelevu. Ambayo inachagiza kujumuisha makundi ya wachache katika maendeleo na kutomwacha yeyote nyuma."