Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Sheria Kenya ziwe kali zaidi kuwalinda wenye ulemavu wa ngozi:Mwaura

Sheria Kenya ziwe kali zaidi kuwalinda wenye ulemavu wa ngozi:Mwaura

Tatizo la ulemavu wa ngozi yaani albino nchini Kenya sio kitu kigeni , lakini ukatili unaoendelea sehemu mbalimbali na Imani potufu dhidi ya watu hao ni masuala yanayotakiwa kukomeshwa.

Wito huo umetolewa na bwana Isaac Mwaura , mbunge anayewakilisha makundi ya walio wachache nchini Kenya.

Amesema hadi sasa nchi hiyo ina sheria za kuwalinda watu wenye ulemavu wa ngozi, lakini sio kali zinahitaji kupigwa msasa

(SAUTI YA MWAURA)