Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zimepigwa lakini bado kuna changamoto kuwalinda Albino:Alshymaa

Hatua zimepigwa lakini bado kuna changamoto kuwalinda Albino:Alshymaa

Kuna mabadiliko kiasi katika uelewa wa kuwalinda watu wenye ulemavu wa ngozi yaani Albino, ingawa safari bado ni ndefu. Hayo yamesemwa na mwanaharakati wa kupigania haki za watu wenye ulemavu wa ngozi Alshymaa Kwegir, mbunge wa zamani wa Tanzania ambaye pia ni mlemavu wa ngozi.

Akizungumza na idhaa hii kutoka kwenye kongamano la kwanza kabisa la kanda ya Afrika kuhusu hatua za kuchukua kulinda watu wenye ulemavu wa ngozi barani humo, ambalo limeingia siku ya pili mjini Dar es Salaam Tanzania. Bi Kwegir akasisitiza

(SAUTI YA ALSHYMAA)

Atoa wito wa juhudi kuongezwa ingawa anatambua vita ni vigumu

(SAUTI YA ALSHYMAA 2)