Sindano ilibadili maisha yangu lakini sina kinyongo- Dkt. Sankok

17 Juni 2016

Kwa siku tatu mfululizo kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa kulifanyika mkutano wa kamati ya mkataba wa kimataifa wa haki za watu wenye ulemavu, CRPD, ukileta pamoja washiriki kutoka nchi wanachama wa Umoja huo. Miongoni mwao alikuwa Dkt. Ole Sankok akiwakilisha jamii ya watu wa asili kutoka Kenya, yeye mwenyewe pia akiwa ni mlemavu wa viungo.

Amina Hassan wa Idhaa hii alipata fursa ya kuzungumza naye masuala kadhaa ambapo Dkt. Sankok hakuchelea kuelezea kile kilichosababisha ulemavu wake kwani alizaliwa mzima. Je nini kilifanyika? na alichukua hatua gani baada ya hali hiyo? Jamii yake je ina mtazamo gani? Ungana basi naye kwenye mahojiano haya hapa akianza kwa kuelezea alivyopata ulemavu wake.

 

♦ Kupata takwimu za waathirika vitani Ukraine bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter