Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Nilipata ulemavu wa kutoona nikiwa na umri wa miaka 16-Dkt. Kabue

Nilipata ulemavu wa kutoona nikiwa na umri wa miaka 16-Dkt. Kabue

Mkutano wa kikao cha tisa cha kamati ya mkataba kuhusu haki za watu wenye ulemavu, CRPD umekamilika wiki hii kwenye makao makuu ya Umoja wa Mataifa. Kikao cha mwaka huu kilikuwa na msisitizo wa kuhakikisha kwamba watu wenye ulemavu wanajumuishwa pia katika utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu SDGs ili kuhakikisha kwamba hakuna mtu anayeachwa nyuma.

Miongoni mwa washiriki katika mkutano huo ni Dkt. Samwel Kabue ambaye anafanya kazi na Baraza la makanisa nchini Kenya. Dkt. Kabue pia amechaguliwa mwanakamati wa CRPD akianza jukumu hilo mwezi Januari mwakani. amehojiwa na Grace Kaneiya wa Idhaa hii akielezea jinsi alivyoapta ulemavu wa macho na hapa anaanza kwa kuelezea kazi anayoifanya.