Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Licha ya ulemavu wa kutoona Dk Macha atimiza ndoto za elimu na kazi

Licha ya ulemavu wa kutoona Dk Macha atimiza ndoto za elimu na kazi

Ulemavu wa kuona haukuwa kikiwazo cha kutimiza ndoto kwa msomi aliye pia mbunge wa viti maalum akiwakilisha kundi la watu wenye ulemavu kutoka Tanzania Dk Elly Macha.

Fuatana na Joseph Msami katika mahojiano ya kusisimua kuhusu visa na mikasa alivyokabiliana navyo hadi kufanikiwa, Dk Macha ambaye alikuwa mjini New York kuhuduhuria mkutano wa mkataba wa nchi wanachama wa watu wenye ulemavu uliomalizika hapo jana.