Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Usaidizi kwa watu wenye ulemavu uendane na mazingira

Usaidizi kwa watu wenye ulemavu uendane na mazingira

Mkutano wa Tisa wa nchi wanachama wa mkataba wa haki za watu wenye ulemavu umetamatishwa huku mmoja washiriki mmasai kutoka Kenya akielezea umuhimu wa kuzingatia tofauti za mazingira katika usaidizi wa kundi hilo.

Akihohijiwa na Idhaa hii, Dkt. Ole Sankok ambaye amewakilisha jamii ya asili amesema ameshuhudia jinsi nchi nyingine zinavyokidhi matakwa ya walemavu mathalani viti mwendo akisema..

(Sauti ya Dkt. Ole)

Lengo la mkutano huo lilikuwa kuangazia umuhimu wa mchango wa watu wenye ulemavu katika kufanikisha malengo ya maendeleo endelevu SDG's.