Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Fedha zinazotumwa na wahamiaji makwao zinaokoa maisha ya mamilioni:IOM

Fedha zinazotumwa na wahamiaji makwao zinaokoa maisha ya mamilioni:IOM

Fedha zilizopatikana kwa jasho na kutumwa na wahamiaji nyumbani kwa familia na jamii zao kila uchao, zinawakilisha msaada muhimu wa kiuchumi kwa mamilioni ya familia zinazohangaika kujikimu kote duniani. Fedha hizi zinainua hali ya maisha kwa njia mbalimbali na zinazsaidia kuzifanya imara jamii zisizojiweza hasa kwa wakati wa msukosuko wa kiuchumi na majanga ya asili nay ale ynayosababishwa na binadamu. Hayo ni kwa mujibu wa mkurugenzi mkuu wa shirika la kimataifa la uhamiaji Lacy Swing.

Ameongeza kuwa fedha hizo zinaongeza kipato cha familia na kukidhi mahitaji ya lazima kama chakula, elimu, nyumba na huduma za afya. Bank ya dunia inakadiria kwamba duniani kote fedha zilizotumwa mwaka 2015 zinadidi dola bilioni 601, huku nchi zinazoendelea zinakadiriwa kupokea dola bilioni 441 katika ya fedha hizo. Bank hiyo imeongeza kwamba idadi ya wahamiaji duniani inatarajiwa kuongezeka hivyo na utumaji wa fedha pia utaongezeka.

Kwa kutambua mchango mkubwa wa wahamiaji kutuma fedha wlikotoka , shirika la IOM ii radhi kuunga mkono “siku ya kimataifa ya Fedha za familia kutoka nje”, iliotangazwa na Mfuko wa Kimataifa wa Maendeleo ya Kilimo (IFAD) leo tarehe 16 Juni.

Ujumbe wa Swing katika siku hii unajikita katika mambo mazuri yatokanayo na fedha hizo, hasa zinavyopatikana, kutumwa na kutumika, akisema mosi, gharama za kutumazipunguzwe na kuimarisha takwimu za utumaji, pili kuboresha fursa ya huduma za fedha, tatu kushirikiana kwa mtazamo wa kujumuisha wadau mbalimbali na kuboresha mazingira ya kupatikana kwa fedha hizo.